International News

Chama tawala cha China, Xi Jinping ashinda muhula Mwingine

Chama tawala cha China, Xi Jinping ashinda muhula Mwingine

Clement Silla

October 25th, 2017

No comments

Rais wa China Xi Jinping ametangaza safu mpya ya uongozi wa kamati kuu ya chama Tawala cha kikomunisti wakati akianza muhula wa mpya wa miaka mitano, akilenga kuimarisha ustawi na kupanua ushawishi wa taifa hilo kimataifa .

Kama ilivyotarajiwa amepewa muhula mwingine kufuatia mkutano wa kwanza wa kamati kuu mpya iliyochaguliwa wakati wa mkutano mkuu wa chama unaofanyika mara mbili katika kipindi cha miaka kumi.

Muundo wa kamati kuu mpya ya chama cha Kikomunisti wenye wajumbe saba unaakisi juhudi za XI kuimarisha umoja kwa kuweka usawa kati ya makundi yenye maslahi tofauti katika chama hicho chenye wanachama zaidi ya milioni 89.

Comments are closed.