International News

Hali ya Dharura yatangazwa Yemeni, Baraza la Usalama latahadharisha kutokea baa la njaa

Hali ya Dharura yatangazwa Yemeni, Baraza la Usalama latahadharisha kutokea baa la njaa

Clement Silla

November 9th, 2017

No comments

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeutaka muungano wa jeshi la nchi za Kiarabu linaloongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen kuondoa vizuizi katika maeneo muhimu ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa tena nchini humo.

Mkuu wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa Mark Lowcock ametahadharisha kutokea kwa baa kubwa la njaa, iwapo misaada haitapelekwa nchini humo kwani hali ya kibinadamu ni ya kutisha.

Saudi Arabia na washirika wake wanaoendesha vita nchini Yemen wamefunga njia zote za ardhini, angani na majini tangu Jumatatu, hatua ambayo imeelezwa na Saudi Arabia kwamba inafuatia mashambulizi ya makombora yaliyorushwa katika mji wa Riyadh na waasi wa Houthi kutoka Yemen.

Comments are closed.