Sports & Entertainment News

Kombe la chalenji kuchezwa Desemba

Kombe la chalenji kuchezwa Desemba

Clement Silla

October 5th, 2017

No comments

Baraza la mashirikisho ya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limethibisha kufanyika kwa mashindano ya Chalenji mwaka huu baada ya kushindwa kuchezwa mwaka jana.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye amesema kuwa mashindano hayo yatafanyika Desemba, lakini nchi wenyeji bado hawajaamua.

Amethibitisha pia mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17yatakayoanza mwezi huu nchini Burundi yatafuatiwa na kombe la chalenji.

Michuano hii inashirikisha nchi 12 ambazo ni Uganda, Sudan, Sudan Kusini, Tanzania, Eritrea, Somalia, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Burundi, Djibouti na Zanzibar.

Comments are closed.