Afrika

Kuapishwa kwa Rais Kenyatta, Viongozi mataifa zaidi ya 11 kuhudhuria sherehe hizo

Kuapishwa kwa Rais Kenyatta, Viongozi mataifa zaidi ya 11 kuhudhuria sherehe hizo

Clement Silla

November 27th, 2017

No comments

Marais 11 kutoka barani Afrika akiwemo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaotarajiwa kushuhudia kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta kuhudumu kwa muhula wa pili na wa mwisho hapo kesho jijini Nairobi.

Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Kimataifa wa Michezo wa Kasarani kuanzia saa mbili asubuhi ambapo wizara ya Mambo ya nje nchini humo, imesema kwamba mataifa mengine 13 yatatuma wawakilishi wao katika sherehe hizo.

Marais ambao wamethibitisha kuhudhuria kuapishwa kwa Kenyatta ni pamoja na rais Yoweri Museveni wa Uganda, rais wa Botswana Ian Khama, Paul Kagame (Rwanda), John Pombe Magufuli (Tanzania),
Edgar Lungu (Zambia), rais wa Djibouti, Namibia, Togo, Somalia na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Kenyatta anatarajiwa kula kiapo na kuanza kuongoza nchi iliyogawanyika kisiasa, huku upinzani ukisema kuwa hautamtambua kama rais wa Kenya huku kiongozi wa upinzani akitarajiwa kuwaongoza wafuasi wake katika mkutano wa hadhara jijini Nairobi.

Comments are closed.