Afrika

Kuelekea uchaguzi wa Urais wa marudio Kenya, Kiongozi wa NASA atangaza maandamano Octoba 26

Kuelekea uchaguzi wa Urais wa marudio Kenya, Kiongozi wa NASA atangaza maandamano Octoba 26

Clement Silla

October 19th, 2017

No comments

Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga, amesema kuwa upinzani utafanya maandamano ya nchi nzima Oktoba 26 siku ya upigaji kura za uchaguzi wa urais wa marudio.

Akihutubia wafuasi wake mjini Nairobi jana Jumatano, Bw. Odinga alisema msimamo wa NASA utaendelea licha ya Tume ya Uchaguzi kusema lazima uchaguzi ufanyike kama iliyopanga.

Wakati hayo yakijiri Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini Kenya Wafula Chebukati amesema hatajiuzulu ingawa mmoja wa Makamishna wa Tume hiyo Roselyn Akombe ametangaza kujiuzulu.

Bwana Chebukati amekiri kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya Tume hiyo na kwamba maelekezo yake ya kisheria kama wakili na Mwenyekiti, yamekuwa hayaungwi mkono na Makamishna ndani ya Tume hiyo na hivyo kumpa hofu kama Uchaguzi huo utakuwa huru na haki, katika kupindi ambacho yeye bado ni Mwenyekiti wa Tume hiyo hususan katika mazingira hayo aliyodai kuwa hivi sasa ni magumu.

Comments are closed.