Afrika

Maandamano nchini Togo, Watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi

Maandamano nchini Togo, Watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi

Clement Silla

October 19th, 2017

No comments

Watu wanne wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya waandamanaji na vyombo vya usalama nchini Togo.

Vifo hivyo vinatokea, huku maandamano yakiendelea kupinga mabadiliko ya katiba kumruhusu Rais Faure Gnassingbe kubakia madarakani hadi mwaka 2030.

Kiongozi huyo amekuwa madarakani tangu mwaka 2003 na familia yake imelitawala taifa hilo la magharibi mwa Afrika tangu mwaka 1968.

Aidha watu wengine 60 wamekamatwa katika mji mkuu, Lome, na mji wa pili kwa ukubwa, Sokode kufuatia vurugu hizo

Comments are closed.