Afrika

Maandamano baada ya uchaguzi yameendelea jana nchini Kenya

Maandamano baada ya uchaguzi yameendelea jana nchini Kenya

Clement Silla

October 31st, 2017

No comments

Maandamano ya baada ya uchaguzi yameendelea jana nchini Kenya, huku waandamanaji wanaoipinga serikali wakipambana na polisi kwenye mji mkuu, Nairobi na mji wa Kisumu ambako ni ngome kuu ya upinzani, baada ya Uhuru Kenyatta kutangazwa mshindi wa uchaguzi mpya wa urais uliofanyika Oktoba 26 kwa kufanikiwa kupata asilimia 98 ya kura.

Waandamanaji walichoma moto matairi na kuwarushia mawe polisi, huku wafuasi wa Kenyatta wakishangilia ushindi huo.

Inakadiriwa watu 66 wameuawa katika ghasia za chaguzi zote mbili, baada ya Mahakama ya Juu kuufuta uchaguzi wa Agosti 8.

Asilimia 40 tu ya Wakenya milioni 19 wanaotakiwa kupiga kura, waliripotiwa kushiriki katika uchaguzi wa marudio ambao ulisusiwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi, Kenyatta aliwashuruku wafuasi wake na alitoa wito wa kuwepo amani na utulivu.

Comments are closed.