Local News

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, ambapo ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, ambapo ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95.

Clement Silla

March 1st, 2019

No comments

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam, ambapo ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana alipotembelea mradi huo ambapo amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi huku akiitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha taratibu za kuutumia uwanja huo ili pindi mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.

Aidha ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri kwa sababu jengo ni zuri na linavutia na amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.

Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Afisa Mtendaji Muu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo limekamilika kwa asilimia 95 na kwamba tayari wamefanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa mbalimbali ambapo mkandarasi anatarajia kukabidhi mradi huo Mei 31 mwaka huu. Jengo hilo lina uwezo wa kubeba abiria milioni sita kwa mwaka.