International News

Majeshi ya Iraq yaanza kuikomboa Raqqa

Majeshi ya Iraq yaanza kuikomboa Raqqa

Clement Silla

October 25th, 2017

No comments

Majeshi ya Iraq yanajitayarisha kuanzisha mashambulizi kukomboa eneo la mwisho la ardhi ya Iraq linalokaliwa na kundi linalojiita dola la Kiislam IS.

Dola la Kiislam limekuwa likirudi nyuma kutokana na mashambulizi makali toka makundi yanayoungwa mkono na Marekani na mashambulizi toka Jeshi la Syria.

Ngome ya Raqqa ilikombolewa na majeshi yanayoungwa mkono na Marekani, na sasa Vikosi vya Serikali ya Iraq vimekuwa vikidondosha vipeperushi vinavyowataka wakazi wa eneo hilo kujitayarisha na mashambulizi ya ukombozi.

Comments are closed.