Local News

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu kuhakikisha zinapeleka vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyozingatia teknolojia mpya.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu kuhakikisha zinapeleka vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyozingatia teknolojia mpya.

Clement Silla

February 27th, 2019

No comments

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza wizara, na taasisi zinazojihusisha na masuala ya elimu kuhakikisha zinapeleka vifaa vya kufundishia na kujifunzia vinavyozingatia teknolojia mpya kulingana na mitaala ya serikali pamoja na kusambaza walimu katika vituo vya wenye uhitaji maalumu nchini ili kusaidia jamii hiyo kupata elimu bora inayokwenda na sambamba na soko la ajira.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi katika manispaa ya Shinyanga anaanza kwa kukagua ujenzi wa jengo la utawala la Mamlaka ya majisafi na usafi wa mazingira Kahama na Shinyanga, KASHWASA kisha kupokea maelezo ya mradi huo ambao hadi sasa umegharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.7.

Akiwa katika chuo cha ualimu cha Shinyanga, SHYCOM, Makamu wa Rais Licha ya kusikitishwa kwa ucheleweshwaji wa kukamilika kwa mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 4.8, unaotekelezwa na Kampuni Afrique construction ltd akapata wasaa wa kusikiliza kero kutoka kwa wanachuo na kuagiza kutolewa ufumbuzi.

Baadae ni katika Maabara ya usanifu wa pamba iliyopo chini ya Bodi ya Pamba ambapo pamoja na kutoa maelekezo mbalimbali ya serikali Naibu waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa akamweleza makamu wa Rais jinsi wizara hiyo ilivyochukua hatua katika kuboresha kilimo cha zao la pamba.

Akifingua bwalo la chakula katika kituo kulea watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija, lililojengwa kwa ufadhili wa kampuni ya Simba logistic, makamu wa rais Sumia Suluhu, ametoa maagizo ya serikali huku naibu waziri wa TAMISEMI, Mwita waitara akiahidi kutafua fedha za kujengwa uzio kwenye majengo hayo mapya.