Afrika

Mapigano nchini Libya, Watu 15 wakiwemo watoto wameuawa

Mapigano nchini Libya, Watu 15 wakiwemo watoto wameuawa

Clement Silla

October 31st, 2017

No comments

Watu 15 wakiwemo watoto wameuawa Mashariki mwa Libya, katika shambulizi la anga lililotekelezwa na jeshi la nchi hiyo katika makabiliano na makundi ya waasi.

Mji wa Derna umekuwa ukilengwa na wanajeshi wa serikali kwa madai kuwa, unawapa hifadhi makundi ya kigaidi.

Hata hivyo jeshi la Libya halijazungumza lolote kuhusiana na shambulizi hilo

Makundi ya waaasi wenye silaha ikiwa ni pamoja na kundi la Islamic State yameendelea kuhatarisaha usalama wa nchi hiyo ambayo ilipoteza mwelekeo tangu kifo cha kiongozi wa taifa hilo Muamar Gaddafi.

Comments are closed.