International News

Matokeo ya awali nchini Japan, Waziri Mkuu Shinzo Abe afanikiwa kutetea nafasi yake

Matokeo ya awali nchini Japan, Waziri Mkuu Shinzo Abe afanikiwa kutetea nafasi yake

Clement Silla

October 23rd, 2017

No comments

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amepata ushindi mkubwa katika uchaguzi ulioitishwa kabla ya wakati wake ambao unampa mamlaka yanayoimarisha msimamo wake ambao tayari ni wa kivita dhidi ya korea kaskazini pamoja na kuuimarisha uchumi wa nchi hiyo ambayo ni wa tatu kwa ukubwa duniani.

Muungano wa kihafidhina wa waziri mkuu Abe unaelekea kupata ushindi wa viti 311 katika bunge lenye viti 465 kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliyochapishwa na kituo binafsi cha televisheni na kumfanya kiongozi huyo kuwa anayeshika madaraka hayo kwa muda mrefu zaidi nchini humo.

Waziri Mkuu Shinzo Abe ameahidi kukabiliana na korea kaskazini baada ya matokeo ya kwanza kuonyesha kuwa ameipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi huo uliofanyika jana

Comments are closed.