International News

Matumizi ya Silaha za Nyuklia, Rais Trump aionya Korea kaskazini asema wala isilijaribu taifa hilo

Matumizi ya Silaha za Nyuklia, Rais Trump aionya Korea kaskazini asema wala isilijaribu taifa hilo

Clement Silla

November 8th, 2017

No comments

Rais wa Marekani Donald Trump ametoa onyo kali kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un kauli ambayo ameitoa katika hotuba ndani ya bunge la Korea Kusini.

Trump amesema kamwe Korea kaskazini isilidharau taifa la Maekani wala kulijaribu
huku akimuonya kiongozi huo wa Korea kaskazini kwamba silaha unazojilimbikizia hazimfanyi kuwa salama lakini zinaweka katika hali hatari zaidi.

Bw. Trump amesema dunia haiwezi kuvumilia hatari inayosababishwa na taifa linaloongozwa na utawala usioaminika ambao unaitishia na silaha za kinyuklia na kuongeza kwamba dunia yote inafaa kuungana kuangamiza utawala wa kikatili wa Korea Kaskazini.

Awali Rais wa Marekani Donald Trump aliitaka Korea Kaskazini kuja kwenye mazungumzo kujadili suala la kuondoa silaha za nyuklia na kusisitiza ulimwengu hususan China na Urusi kuiwekea shinikizo kali Pyongyang kusitisha utengenezaji wake wa silaha za kinyuklia.

Rais Donald Trump amehitimisha ziara ya siku mbili nchini Korea Kusini katika ziara ya siku tano barani Asia na hvi sasa anaelekea nchni China.

Comments are closed.