International News

Mgogoro wa Mynmar, Wabunge wa marekani wataka kurejeshwa vikwazo vya nchi hiyo

Mgogoro wa Mynmar, Wabunge wa marekani wataka kurejeshwa vikwazo vya nchi hiyo

Clement Silla

October 19th, 2017

No comments

Wabunge kadhaa wa Mareani wameutaka utawala wa Rais Donald Trump kurejesha vikwazo vya usafiri dhidi ya viongizi wa kijeshi wa Mynmar kuhusiana na vile wanavyowatendea waislam wa Rohingya nchini Mynamar.

Mynamar imekana madai ya safisha safisha ya kikabila ya mauaji holela dhidi ya kundi hilo la kikabila ambapo mamia kwa maelfu wamekibia kutoka jimbo la Rakhine na kukimbia nchi jirani ya Bangladeshi.

Wabunge 43 kutoka chama cha Republican na Democratic katika baraza la wawakilishi la Marekani wameonya kwamba maafisa katika nchi hiyo wanaelekea kukana juu ya kile kinachotokea licha ya kwamba uliwengu mzima umesikitishwa na hilo.

Marekani na umoja wa Ulaya zimekuwa zikitafakari kuweka vikwazo vinavyolenga maeneo maalumu lakini wana wasiwasi wa kuathiri uchumi wa nchi hiyo kudhoofisha mahusiano ambayo tayari ni wasiwasi kati ya kiongozi wa Mynamr AungSan Suu Kyi na jeshi.

Comments are closed.