International News

Mgogoro wa Catalonia, Muungano wa vyama vya wfanyakazi washinikiza maandamano

Mgogoro wa Catalonia, Muungano wa vyama vya wfanyakazi washinikiza maandamano

Clement Silla

November 8th, 2017

No comments

Muungano wa vyama vya wafanyakazi katika eneo la Catalonia umewatolea wito wakazi wa eneo hilo kumiminika mitaani leo huku mkutano mkubwa unaounga mkono uhuru wa eneo hilo ukitarajiwa kufanyika mjini Barcelona.

Hayo yanajiri wakati ambapo mzozo wa kisiasa unaendelea kushuhudiwa nchini Uhispania na kuvuruga kabisa mustakabali wa taia hilo..

Wakati huo huo Mahakama ya Brussels inatarajiwa kumsikiliza aliyekuwa rais wa Catalonia Carles Puigdemont na wajumbe wanne wa serikali yake.

Wanaharakati hao wako uhamishoni nchini Ubelgiji, baada ya kufutwa kazi na serikali kuu ya Uhispania ikiungwa mkono ba bunge la nchi hiyo.

Kuna hatari Carles Puigdemont na wenzake wanne kurudishwa nchini Uhispania ili wajibu shutma dhidi yao.

Viongozi hawa wa zamani wa Catalonia wanashtumiwa uchochezi na uasi, baada ya eneo hili kujitangazia uhuru, uliopingwa na serikali kuu ya Uhispania.

Comments are closed.