Afrika

Mchakato wa kuelekea uchaguzi wa marudio Kenya, Muungano wa NASA wasitisha maandaano kwa siku ya leo

Mchakato wa kuelekea uchaguzi wa marudio Kenya, Muungano wa NASA wasitisha maandaano kwa siku ya leo

Clement Silla

October 17th, 2017

No comments

Muungano wa Upinzani nchini Kenya National Super Alliance (NASA) umesitisha maandamano ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika nchini humo leo kushinikiza mabadiliko katika tume ya uchaguzi licha ya kwamba jana yalifanyika katika miji kadhaa ikiwemo Mombasa.

Katika taarifa yake, muungano huo unaoongozwa na waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umesema umechukua hatua hiyo kupata fursa ya kuomboleza watu ambao wameuawa kwenye maandamano ya awali ya wafuasi wake.

NASA wameahidi kufanya maandamano kila siku kushinikiza mabadiliko katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mpya wa urais uliopangwa kufanyika Octoba 26.

Taarifa iliyotumwa na Dennis Onyango ambaye ni msemaji wa Bw. Odinga imesema maandamano hayo yataanza tena hapo kesho Octoba 18.

Comments are closed.