Local News

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Februari 28 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) . Kazuhiko Koshikawa.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo Februari 28 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) . Kazuhiko Koshikawa.

Clement Silla

February 28th, 2019

No comments

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro na Balozi wa Japan hapa nchini Shinichi Goto.

Rais Magufuli ameishukuru JICA kwa kuwa mdau muhimu wa maendeleo ya Tanzania na amemhakikishia Bw. Koshikawa kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano huo hususani katika ujenzi wa miundombinu ambapo tayari miradi kadhaa imetiwa saidi ikiwemo upanuzi wa barabara ya Mwenge – Morocco (kilometa 4.3) na Daraja la Gerezani Jijini Dar es Salaam ambayo ujenzi wake utaanza wakati wowote kuanzia sasa.

Kwa upande wake Bw. Koshikawa amempongeza Rais Magufuli na Serikali ya awamu ya tano kwa juhudi kubwa za kukuza maendeleo ya Tanzania na kuendeleza ushirikiano mzuri na JICA uliowezesha miradi mingi ya maendeleo kutekelezwa.

Aidha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro amesema ushirikiano mzuri wa Serikali ya Tanzania na JICA unathibitisha rekodi nzuri ya uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi mbalimbali ambao una manufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania.

Wakati huyo huo Rais Magufuli ameagana na Mwakilishi Mkazi wa JICA hapa nchini aliyemaliza muda wake Toshio Nagase na kumkaribisha Mwakilishi Mkazi mpya wa JICA Naofumi Yamamura.