Local News

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Machi, 2019 ameungana na Waumini wa Kanisa Katoliki katika Misa Takatifu ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Jijini Dar es Salaam.

Clement Silla

March 6th, 2019

No comments

Misa hiyo imeongozwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph Padre Joseph Mosha.

Mhe. Rais Magufuli amehudhuria misa hiyo akiwa na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.

Jumatano ya Majivu ni kuanza kwa kipindi cha Kwaresma ambapo Wakristo huingia katika mfungo na maombi ya kumbukumbu ya mateso ya Bwana Yesu Kristo na kipindi hiki humalizika siku ya Pasaka ambayo ni maadhimisho ya ufufuko wa Yesu Kristo.