Afrika

Shambulizi la bomu la kutegwa Somalia, Mamlaka za Usalama zaendelea kutafuta miili ya waliofunikwa na vifusi

Shambulizi la bomu la kutegwa Somalia, Mamlaka za Usalama zaendelea kutafuta miili ya waliofunikwa na vifusi

Clement Silla

October 17th, 2017

No comments

Mamlaka za usalama nchini Somalia zimesema kwamba idadi ya watu waliouawa baada ya bomu kulipuka kwenye lori katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu mwishoni mwa wiki huenda ikawa zaidi ya tatu.

Shambulizi hilo linaelezewa kuwa baya zaidi kuwahi kutokea kwenye eneo lote la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo Takribani watu 400 walijeruhiwa na wengine 70 hawajulikani walipo baada ya kufukiwa na vifusi kufuatia mlipuko huo uliolengwa dhidi ya umati wa watu.

Kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye kufungamana na al-Qaida, linatajwa kuhusika ingawa halijatoa tamko
kukiri. Kundi hilo limekuwa na historia ya kufanya mashambulizi nchini humo.

Kufuatia shambulizi hilo Rais wa Marekani  Donald Trump ameapa kuongeza mapambano dhidi ya kundi hilo la kigaidi huku  Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed akitangaza operesheni mpya ya kijeshi dhidi ya Al shaabab.

Somalia imetangaza siku tatu za Maombolezo  kufuatia mauaji hayo, huku  ikiomba wananchi kujitolea damu ili kusaidia majeruhi wenye uhitaji.

Comments are closed.