Local News

RAIS wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein amewataka wananchi kisiwani Pemba kuendelea kuiunga Mkono serikali katika kulinda miundombinu dhidi ya hujuma za baadhi ya wachache ili iweze kudumu.

RAIS wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein amewataka wananchi kisiwani Pemba kuendelea kuiunga Mkono serikali katika kulinda miundombinu dhidi ya hujuma za baadhi ya wachache ili iweze kudumu.

Clement Silla

February 25th, 2019

No comments

Akizungumza na wananchi wa wilaya chakechake baada ya kuzindua kituo cha Afya Ngomeni, Dkt Shein ameahidi kufuatilia ili kujua gharama zilizotumika katika ujenzi wa kituo hicho.

Mapema waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa , Serikali za Mitaa na Idara Maalumu za SMZ Haji Omar Kheir alisema sehemu kubwa ya uchumi zanzibar umetoka Ngomeni , huku waziri wa Ujenzi , Mawasiliano na Usafirishaji Sira Ubwa Mwamboya akisema serikali inachukua hatua za kuendeleza ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika viiwa vya Unguja na Pemba.
Katika ziara hiyo pia Dkt Shein amezindua barabara ya Mgomeni Kiuyuni iliyojengwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Comments are closed.