International News

Siasa za Marekani na Njama za Rushwa, Mwenyekiti wa kampeni za Donald Trump matatani

Siasa za Marekani na Njama za Rushwa, Mwenyekiti wa kampeni za Donald Trump matatani

Clement Silla

October 31st, 2017

No comments

Mjumbe wa tume maalum ya uchunguzi nchini Marekani, Robert Mueller na timu yake, wametangaza mashtaka ya kwanza dhidi ya Paul Manafort, aliyekuwa mwenyekiti wa kampeni ya Rais wa Marekani, Donald Trump, mshirika wa kibiashara wa Manafort, Rick Gates na aliyekuwa mshauri wa kampeni, George Papadopoulos.

Mashtaka hayo ni pamoja na kutakatisha fedha haramu na njama dhidi ya Marekani.

Manafort na Gates jana wamekana mashtaka 12 ya uhalifu yanayowakabili, ingawa mapema mwezi huu wa Oktoba Papadopoulos alikiri mashtaka dhidi yake kwa kulidanganya Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI.

Hata hivyo Jaji wa mahakama moja mjini Washington ameamuru Manafort na Gates wawekwe katika kifungo cha nyumbani.

Papadopoulos alikamatwa mwezi Julai ingawa msemaji wa Ikulu ya Marekani, Sarah Sanders amesema matukio ya hivi karibuni hayaonyeshi ushahidi kuhusu ushirikiano kati ya timu ya kampeni ya Trump na Urusi.

Comments are closed.