Afrika

Watu kumi na tano wauwawa katika shambulio la bomu nchini Somalia.

Watu kumi na tano wauwawa katika shambulio la bomu nchini Somalia.

Clement Silla

March 29th, 2019

No comments

 

Polisi nchini Somalia imesema Watu kumi na tano wameuawa katika shambulio la bomu lililotegwa katika gari ndogo karibu na hoteli na migahawa miwili mjini Mogadishu nchini Somalia ambapo Wanawake watano ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Idara ya magari ya wagonjwa Abdikadir Abdirahman ameliambia Shirika la Habari la Reuters kuwa idadi ya watu waliouawa kwa sasa ni kumi na tano ikiwa ni pamoja na wanawake watano, na majeruhi 17
Hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.

Hivi karibuni waasi wa kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al Shabab waliendesha shambulio lililolenga hoteli Wehliye ambayo ilishambuliwa Hoteli hiyo ambayo inapatikana katika mtaa wa Maka al Moukaram, mtaa ambao ni maarufu mjini Mogadishu.