Sports & Entertainment News

Ubaguzi wa rangi waiweka pabaya timu ya Lazio nchini Italia

Ubaguzi wa rangi waiweka pabaya timu ya Lazio nchini Italia

Clement Silla

October 6th, 2017

No comments

Chama cha soka nchini Italia kimeipa adhabu klabu ya Lazio kwa kitendo cha ubaguzi wa rangi baada ya mashabiki wake kumzomea Claud Adpajong wa klabu ya Sossulo na hivyo itawalazimu kucheza michezo yao miwili huku milango ya uwanja ikiwa imefungwa tena bila mashabiki.

Mchezo wa kwanza ni pale watakapoikaribisha Cagliari tarehe 22 na pia watakapoikaribisha Udinesse November 5, michezo yote hii miwili itachezwa bila mashabiki kuwepo uwanjani.

Lazio ni kati ya vilabu ambavyo vinafanya sana matukio ya ubaguzi wa rangi kwani hata Antonio Rudiger wakati yuko Serie A alifanyiwa vitendo vya namna hii na mashabiki wa Lazio pamoja na kiungo wao Senad Lulic.

CHANZO : CRI KISWAHILI

Comments are closed.