Local News

Ubelgiji imesema itaendelea kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika nyanja za kiuchumi na kimaendeleo ikiwa ni azma yake kuunga mkono mikakati inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Ubelgiji imesema itaendelea kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika nyanja za kiuchumi na kimaendeleo ikiwa ni azma yake kuunga mkono mikakati inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano.

Clement Silla

February 25th, 2019

No comments

Ubelgiji imesema itaendelea kudumisha Ushirikiano na Tanzania katika nyanja za kiuchumi na kimaendeleo ikiwa ni azma yake kuunga mkono mikakati inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano ya kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi pamoja na miradi mikubwa ya Kimaendeleo ikiwemo ya Miundombinu.

Balozi wa ubelgiji hapa nchini Peter Van Acker pamoja na Mkurugenzi wa maendeleo wa serikali ya Ubelgiji katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara Jozef Smets,wamesema hayo wakati walipokutana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi- CCM Dk.Bashiru Ally katika ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini dar es salaam ambapo wamesema Ushirikiano baina ya Tanzania na Ubelgiji ni muhimu katika kuwaletea wananchi maendeleo pamoja na kuimarisha uwekezaji na Utalii.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Ubelgiji pamoja na nchi nyingine za ulaya na Marekani ambazo zimeonyesha nia ya kuendelea kuunga Mkono mikakati ya serikali ya kuimarisha utoaji huduma na maendeleo kwa wananchi wa Tanzania.

Comments are closed.