Sports & Entertainment News

Uhamisho wa wachezaji Ulaya

Uhamisho wa wachezaji Ulaya

Clement Silla

August 17th, 2017

No comments

West Brom wamemnunua kiungo wa kati wa zamani wa England Gareth Barry kutoka Everton kwa bei ambayo haijafichuliwa. Mchezaji huyo wa miaka 36 amecheza mechi 628 katika Ligi ya Premia katika misimu 21 akichezea Aston Villa, Manchester City na Everton.
Barry sasa anahitaji kucheza mechi tano zaidi pekee kuvunja rekodi ya nyota wa Manchester United Ryan Giggs ya mechi 632.

Wakati huo huo mchezaji Gylfi Sigurdsson amekihama klabu ya Swansea na kujiunga na Everton. Nyota huyo kutoka Iceland amesajiliwa kwa jumla ya pauni milioni 45 za Uingereza ambacho ndio kiwango cha juu kwahi kutumiwa na Everton kusajili mchezaji.

Klabu ya machester city kwa upande mwingine bado wanawasaka wachezaji kadhaa kabla ya kufungwa kwa dirisha la uamisho wa wachezaji Agosti 31. KLabu hiyo inayoongozwa na Pep Guardiola sasa inamtaka beki wa zamani wa Manchester United Johny Evans anayesakata soka yake West Brom hila klabu hiyo imekataa pauni milioni 18 za Uingereza iliyotolewa na Man City.

CHANZO : CRI KISWAHILI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *