Afrika

Uteuzi wa rais Mugabe kuwa Balozi wa amani WHO, yakubali kumtengua baada ya minong’ono mingi

Uteuzi wa rais Mugabe kuwa Balozi wa amani WHO, yakubali kumtengua baada ya minong’ono mingi

Clement Silla

October 23rd, 2017

No comments

Hatimaye Zimbabwe imekubali uamuzi wa shirika la Afya duniani kumvua rais Robert Mugabe wadhifa wa balozi mwema wa shirika hilo ambapo taarifa hiyo imetolewa na waziri wa mambo ya nje wa Zimbabwe Walrter Mzembi
Akitangaza hatua hiyo ya shirika la WHO mkuu wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus ameseka amesikiliza vizuri wale wote ambao wameelezea hisia zao kuhusiana na uteuzi huyo na hivyo kuchukua maamuzi ya kutengua.

Uteuzi wa Bw.Mugabe ulipatwa na shutuma kali ambapo Serikali ya Uingereza Waziri mkuu wa Canada na mashirika mengine kadhaa pamoja na watumaiji wa mitandao ya kijamii walikosoa uteuzi huo hatua iliyofanya shirika hilo kutengua uteuzi huyo.

Comments are closed.