International News

Azma ya jimbo la Catalonia kujitenga, Waziri Mkuu wa Uhispania atangaza kuchukua hatua madhubuti zaidi

Azma ya jimbo la Catalonia kujitenga, Waziri Mkuu wa Uhispania atangaza kuchukua hatua madhubuti zaidi

Clement Silla

October 23rd, 2017

No comments

Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy ametangaza hatua anazokusudia kuzichukua ili kulisambaratisha vuguvugu la wanadai kujitenga kwa jimbo tajiri la Catalonia.

Bwana Rajoy ametoa wito kwa bunge la Uhispania kutumia ibara ya katiba ya Uhispania ambayo haijawahi kutumiwa inayoiruhusu serikali kuu kuingilia kwa muda usimamizi wa jimbo ikiwa viongozi wa jimbo hilo wamekikuka sheria.

Uhamasishaji wa mamlaka hiyo ya kikatiba inayotolewa na ibara ya 155 ya katiba ya Uhispania ndiyo hatua thabiti zaidi iliyochukuliwa na serikali ya Uhispania mpaka sasa kuhusiana na azma ya viongozi wa Catalonia kutangaza uhuru kwa msingi wa kura ya maoni iliyofanyika Octoba 1 ambayo hata hivyo mahakama iliitangaza kura hiyo kuwa batili.

Comments are closed.