Local News

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara kupeleka muswada Bungeni kwa ajili ya kuunganisha Taasisi mbili za Serikali ambazo ni TBS na TFDA kutokana na Taasisi hizo kufanana katika utendaji kazi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara kupeleka muswada Bungeni kwa ajili ya kuunganisha Taasisi mbili za Serikali ambazo ni TBS na TFDA kutokana na Taasisi hizo kufanana katika utendaji kazi.

Clement Silla

February 28th, 2019

No comments

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara kupeleka muswada Bungeni kwa ajili ya kuunganisha Taasisi mbili za Serikali ambazo ni Shirika la Viwango Tanzania TBS pamoja na Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA kutokana na Taasisi hizo kufanana katika utendaji kazi pamoja na kupunguza urasimu uliolalamikiwa kwa muda mrefu na Wafanyabishara nchini unaofanywa na taasisi hizo.

Akizungumza katika mkutano uliomkutanisha Wafanyabishara kutoka Wilaya ya Ilala, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wafanyabishara kuhusu utozwaji tozo wa Taasisi hizo pamoja na suala la ucheleweshwaji wa vipimo vya sampuli za bidhaa vitu ambavyo vimekuwa vikimuumiza Mfanyabishara na kuzorotesha shughuli za uzalishaji.

Aidha Waziri Mkuu amevitaka vyombo hivyo vya Serikali pamoja na vingine vinavyosimamia Sekta ya Biashara kuhakikisha vinapitia Sheria na kanuni zinazosimamia biashara ili zisilete usumbufu kwa wafanyabiashara sambamba na kutumia lugha nzuri na mapokezi ya kutia hamasa mfanyabishara pamoja na kuanzisha utaratibu kwa watendaji kutembelea maeneo ya wafanyabishara ili kujua changamoto zao na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanada na Biashara Joseph Kakunda amekiri kuwepo kwa tozo nyingi kwa wafanyabishara ambazo zinaathiri ustawi wa bishara nchini sambamba na kufungwa kwa biashara nyingi.

Awali baadhi ya wafanyabishara walippata nafasi ya kuelezea changamoto wanazokutana nazo katika biashara ikiwemo utitiri wa kodi,ukaguzi wa bidhaa unavyochukua muda mrefu kupitia mamlaka husika,vitendo vya rushwa kwa baadhi ya watumishi wa taasisi za umma.