Local News

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha watu wote waliowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha watu wote waliowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.

Clement Silla

February 25th, 2019

No comments

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza viongozi na wazazi wilayani Siha mkoani Kilimanjaro washirikiane kuhakikisha watu wote waliowapa mimba wanafunzi wanasakwa na kufikishwa kwenye vyombo vya dola, ambapo amesema katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana, wanafunzi wa kike 57 walikatishwa masomo baada ya kupata mimba na hadi sasa kesi zilizofunguliwa ni sita tu.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Isanja, Sanya Juu wilayani Siha wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro jana.

Amesema Serikali imeweka sheria kali ya kumlinda mtoto wa kike lengo likiwa kumuwezesha amalize masomo yake ili aweze kujikwamua kiuchumi na aondokane na utegemezi, hivyo ni marufuku kuwakatisha masomo na kwamba watoto wa kike wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii na adhabu kali itatolewa kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako na katika nyumba ya wageni.

Waziri Mkuu amewatahadharisha wazazi au walezi watakaowaozesha watoto wa kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria huku akiwataka wanafunzi wote hususani wa kike wasome kwa bidii ili watimize ndoto zao na wasikubali kushawishika kwa sababu watashindwa kuendelea na masomo yao.

Comments are closed.