International News

Ziara ya Rais Trump Barani Asia, Mazungumzo juu ya vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini yatawala

Ziara ya Rais Trump Barani Asia, Mazungumzo juu ya vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini yatawala

Clement Silla

November 9th, 2017

No comments

Marekani na China zimeahidi kushirikiana kwa karibu katika mzozo wa Korea Kaskazini, biashara, dawa za kulevya na utulivu wa kimataifa.

Katika mazungumzo yao ya leo walipokutana mjini Beijing, Rais Xi Jinping wa China amemwambia mwenzake wa Marekani, Donald Trump, kwamba China inaamini ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ndiyo chaguo pekee sahihi na kwamba uhusiano wao umeingia katika mwanzo mpya wa kihistoria, kwa maslahi ya watu wa nchi hizo pamoja na amani, ustawi na utulivu wa dunia.

Kwa upande wake Trump amesema wana uwezo wa kutatua matatizo ya dunia kwa miaka mingi inayokuja na ameitaka China kuishinikiza Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia.

Aidha, Rais Trump na Rais Xi wameahidi kuleta utulivu duniani, hasa Afghanistan na wamethibitisha kujizatiti kupambana na biashara ya kimataifa ya dawa za kulevya.

Comments are closed.